Sunday, April 28, 2024
HomeTop NewsMilioni 130 za NMB kusapoti bonanza la Wabunge Leo

Milioni 130 za NMB kusapoti bonanza la Wabunge Leo

Meneja wa NMB Kanda ya Kati ,Janeth Shango (wapili kulia) akimkabidhi jezi za michezo mbalimbali Mwenyekiti wa Bunge Bonanza ,Festo Sanga (kushoto), makabidhiano hayo yalifanyika Bungeni Dodoma jana ,NMB ilikabidhi vifaa hivyo vyote vikiwa na thamani ya sh milioni 130, kulia ni Meneja wa NMB Tawi la Bunge ,Grace Matemu

Mwandishi Wetu,Dodoma

BENKI ya NMB jana imekabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh90 Milioni kwa
Timu ya Bunge huku wakisisitiza umuhimu wa mashirikiano.
Vifaa vilivyokabidhiwa ni furana, traksuti na vifaa vingine vya michezo lakini NMB
walikubali kutoa kifungua kinywa kwa wabunge wote na wageni pamoja na kuwawekea
mahema kwaajili ya kukutumika katika bonanza hili ambapo ufadhili huo kwa ujumla
wake unagharimu Sh130 milioni.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa mweneyekiti wa Bunge Bonanza Mheshimiwa Festo Sanga,
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Kati, Janeth Shango alisema wanatoa vifaa hivyo
katika muendelezo na utaratibu wao kwa taasisi za Serikali na wadau wengine kwani
ndiyo utaratibu waliojiwekea.
Shango alisema utoaji wa vifaa hivyo siyo mara ya kwanza na haitakuwa mwisho kwani
wanaendelea kuamini kuwa, Taifa bora ni lile linalojali afya za watu wake ikiwemo
kwenye michezo. 
Meneja huyo wa kanda ya kati aliwaomba wabunge kuendeleza mashirikiano na benki
hiyo kwa kuwa ni wadau ambao wanapaswa kufanya shughuli zao kwa pamoja kwani
wote wanawahudumia wananchi.
“Lakini tuwaombe wabunge na wananchi kuendelea kuitumia benki yenu ya NMB kama
ambavyo tumeendelea kuwa wamoja na sisi tunaahidi kuwa pamoja nanyi kwa kila
jambo ili mradi tujenge nchi yetu kwa kuwa na watu wenye afya njema,” alisema
Shango.
Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo, Mwenyekiti wa Bonanza la Bunge Fessto
Sanga alisema msaada huo kutoka NMB siyo mara ya kwanza kwani hata kwa mwaka
huu imekuwa ni mara ya pili wakiwafadhiri.
Alisema katika bonanza la kwanza walipokea vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Sh100
milioni jambo linalofanya kwa mwaka huu pekee kuwa wamepata ufadhiri wa zaidi ya
Sh230 milioni kutoka benki hiyo.
Sanga alisema vifaa vilivyotolewa na NMB vinawasaidia kwenye mabonanza yao
ikiwemo michezo itakayofanyika leo (Septemba 2,2023) ambalo ni maalumu kwa
mashindano ya wabunge na watumishi wa ofisi ya bunge.
Kwa upande wa wabunge watashirikiana na wenzao wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
na michezo itaanzia Chuo cha Mipango Dodoma kuelekea Viwanja vya Jonmerini.
Mbunge huyo wa Makete alisema mgeni rasmi katika bonaza hilo lenye lengo la
kupambana na magonjwa yasiyo na kuambukiza atakuwa Spika wa Baraza la
Wawakilishi Zuber Ali Maulid.
Mwenyekiti huyo alitaja michezo itakayokuwepo katika bonanza hilo ni Mpira wa
miguu,pete,bao,kukimbia,mwendokasi,kupita kwenye pipa na mingine.

RELATED ARTICLES

Most Popular