Thursday, December 7, 2023
HomeTop NewsVigogo wa Serikali wafurika Rais Samia akizindua Tawi la 230 la NMB

Vigogo wa Serikali wafurika Rais Samia akizindua Tawi la 230 la NMB

NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 30,
amezindua Tawi la Benki ya NMB Paje, Mkoa wa Kusini Unguja, hapa Zanzibar,
uzinduzi unaoendelea kupanua mtandao wa matawi ya benki hiyo nchini na kufikia 230,
yanayohudumia zaidi ya Wateja Milioni 6.
Uzinduzi huo ambao ni sehemu ya Tamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Festival 2023),
ulioweka rekodi ya mahudhurio makubwa ya viongozi waandamizi wa Serikali na
wastaafu, umekuja siku 58 tangu Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango alipozindua tawi
la 229 la Benki ya NMB Buhigwe mkoani Kigoma.
Rekodi ya mahudhurio makubwa ya viongozi waandamizi wa Serikali imewekwa katika
uzinduzi wa NMB Paje, ambako ukiondoa Rais Samia, wengine waliohudhuria ni
pamoja Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Gavana Benki Kuu ya Tanzania (BoT),
Emmanuel Tutuba na Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba
Viongozi wengine ni Spika  wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia
Ackson, Msemaji wa Serikali, Gerson Msigwa, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Moses
Kusiluka, Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mizengo Pinda, pamoja na Mawaziri
wa Wizara mbalimbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ).
Rais Samia aliwasili tawini NMB Paje majira ya saa 10:15 alasiri na ilimchukua dakika
chache Bi Zaipuna kumpa maelezo mafupi ya tawi hilo na NMB kwa ujumla, ambako
alimweleza kuwa tawi hilo linaenda kumaliza changamoto ya wakazi wa Paje kusafiri
umbali wa kilomita 60 kufuata huduma zetu za kibenki kwenye Tawi la
Mwanakwerekwe.
“Karibu kutuzindulia Tawi la NMB Paje, ambalo ni la nne hapa visiwazi Zanzibar, lakini
likiwa ni la 230 kwa mtandao mzima wa matawi yetu nchini Tanzania. 
“Tuna imani kwamba tawi hili linaenda kuwasaidia sana wakazi wa mahali hapa, ambao
awali walikuwa wanasafiri umbali mrefu wa takribani kilomita 60 kwenda
Mwanakwerekwe kufuata huduma zetu za kibenki katika tawi letu kule.
“Tawi hili litatoka huduma zote za kifedha ikiwamo kufungua akaunti, kufanya malipo,
kuweka ama kutoa fedha, huduma za bima, mikopo, pamoja na kubadili fedha za
kigeni. 
“Pia, wafanyakazi wetu wa tawi hili watatumia jengo hili kutoa Elimu ya Fedha kwa
wananchi hasa wavuvi, wakulima wa mwani na wazalishaji chumvi, elimu ambayo tayari
imeshaanza kutolewa hapa kabla hata ya uzinduzi huu unaofanyika leo,” alisema Bi.
Zaipuna kumueleza Rais Samia.

Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan(watatu kushoto) akifurahia jambo baada ya kuzindua rasmi tawi la NMB Paje huko Zanzibar. Tawi la Paje linakuwa tawi la 230 la Benki ya NMB nchini Tanzania na la nne kwa Zanzibar. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango wa Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya, wapili kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, watatu kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB, Dkt. Edwin Mhede, wapili kushoto ni Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba na kushoto ni Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Emmanuel Tutuba

Baada ya maelezo hayo, Mheshimiwa Rais alikata utepe kuashiria ufunguzi wa tawi
hilo, kabla ya kuingia ndani kukagua miundombinu na Mifumo ya utoaji huduma ndani
ya jengo hilo.
Akiwa ndani ya tawi, Rais Samia alitembezwa katika Ofisi za Vitengo na Idara
mbalimbali, zoezi lililofanyika kwa dakika 15, kabla ya kuondoka hapo na kuingia
kwenye Viwanja vya Paje, vilivyopo mita 50 tu kutoka hapo, alikozungumza na
wananchi wakati wa kuubariki Usiku wa Samia, ambao ni sehemu ya Kizimkazi Festival.
Tawi la NMB Paje linakuwa ni la tatu kufunguliwa na benki hiyo mwaka huu 2023,
likitanguliwa na matawi ya Kwa Mrombo jijini Arusha (Mei 3) na Buhigwe Kigoma (Julai
4).

RELATED ARTICLES

Most Popular