Watani wa jadi kutoka mitaa ya Kariakoo Simba SC na Yanga SC wamekipiga leo kwenye dimba la Benjamin Mkapa Dar es salaam, ambapo Yanga wameibuka kidedea dhidi ya Wekundu hao wa Msimbazi kwa goli moja kwa sifuri.
Goli hilo ambalo limefungwa mnamo dakika za majeruhi na Kelvin Kijili, limeinua shangwe na furaha kwa mashabiki wa Yanga SC.
Kwa upande wa kocha wa Simba Fadlu Davids amesema, Timu yake inaendelea kupata uzoefu licha ya kufungwa kwenye mechi ya leo, pia anaelekeza matumaini zaidi kwenye dirisha lijalo la usajili.
Kocha wa Yanga Miguel Gamondi amewapongeza wachezaji wake huku akisema kipindi cha kwanza walicheza kimkakati wakijua Simba wataingia kwa kasi. Pia amempongeza kocha wa Simba Fadlu Davids akisema amebadilisha timu hiyo kwa kiasi kikubwa.