Wanafunzi wa wawili wa Sekondari huko mkoani Tabora, wamefukuzwa shule kwa makosa ya kufanya mchezo mchafu na kujirekodi picha za utupu na kuzisambaza.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Paul Matiko Chacha amesema “Majuzi watoto kama hawa pale Kazima Sekondari, hayo unayoyazungumza tumefukuza watoto wawili wa kike wakifanya mchezo mchafu wakijirekodi, tukaita wazazi wao tukawaambia haya ndio watoto wenu wanayoyafanya, mtoto mmoja akitokea misumbwi mwengine urambo, tukawaambia hizi sio tabia za Kitandzania hawa kama walijifunza huko ondokeni nao”.
Ili kudhibiti matukio hayo na mtakukio ya kijinsia ya wanafunzi wakiwa katika shule ya sekondari Mwayunge iliyopo wilayani Igunga, Waziri wa Maendeleo ya Jamii Dk. Doroth Gwajima amewataka maafisa ustawi wa jamii maendeleo ya jamii na maafisa elimu wote nchini kuimarisha madawati ya ulinzi kwa watoto mashuleni.