Thursday, December 7, 2023
HomeTop NewsUzinduzi wa jengo la PAPU Arusha

Uzinduzi wa jengo la PAPU Arusha

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella amewakaribisha wananchi wa jiji la Arusha kushiriki uzinduzi wa jengo la Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Posta Afrika (PAPU) lililopo barabara ya Moshi, mtaa wa Sekei jirani na hoteli ya Mount Meru.

Mhe. Mongela ametoa mwaliko huo leo Septemba mosi, 2023 jijini Arusha ambapo ametoa taarifa ya Mgeni rasmi atakayezindua jengo hilo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 2 Septemba, 2023.

Akizungumza jana jijini humo, Mkuu wa Mawasiliano na Itifaki kutoka Umoja wa Posta Afrika (PAPU), Bw. Faustine Oyuke amesema kuwa Umoja wa Afrika umejenga jengo hilo kwa lengo la kuhakikisha Sekta ya Posta inaboreka na kukuza uchumi wa kidijitali.

“Vilevile ni kuhakikisha jengo hili linakuwa kitovu cha taaluma ya Sekta ya Posta kwasababu kuna ukumbi maalum wa mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa wataalamu wa Sekta ya Posta barani Afrika ambao ni nchi wanachama na marafiki wa umoja huo ili kuja kujifunza kwa namna gani sekta hiyo inakuwa chachu ya maendeleo barani Afrika.”, amesema Bw. Oyuke.

Jengo hilo la PAPU pia lina Migahawa ya kisasa na kumbi kubwa za kisasa za mikutano pamoja na sehemu nyengine za huduma za kifedha.

RELATED ARTICLES

Most Popular