Dodoma, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini “Rural Energy Agency” (REA) Hassan Saidy amesema wameanza utekelezaji wa mradi wa kusambaza Gesi ya majumbani (ya kupikia LPG) 71,000 yenye thamani ya shilingi bilioni tatu sambamba na majiko laki mbili.

Mhandisi Hassan amesema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini kwa kushirikiana na Benki ya Dunia (WB) imetenga kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni sita kwa ajili ya mradi huo wa kusambaza majiko vijijini. Pia amesema ya kwamba jumla ya takribani Shilingi Bilioni 10 ambazo ni za mwaka wa bajeti 2023/24 zimetengwa kwa ajili ya kufanikisha mradi huo.