Thursday, December 7, 2023
HomeTop NewsElimu ya Msingi mwisho darasa la Sita

Elimu ya Msingi mwisho darasa la Sita

Taasisi ya Elimu Tanzania imetoa mtaala mpya wa elimu ya msingi kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba. Muundo wa mtaala unaonesha elimu hiyo ya msingi itatolewa kwa awamu mbili, Ya kwanza ni kuanzia darasa la kwanza mpaka la pili huku ukijikita kwenye Kusoma, Kuhesabu na Kuandika (KKK). Mtaala umezingatia maeneo ya kujifunza kwa darasa la kwanza na la pili kwenye ujenzi wa lugha, utamaduni, mawasiliano na stadi za hisabati, sanaa, michezo na afya pamoja na mazingira.

Na kwenye awamu ya pili itaendelea kwenye darasa la tatu mpaka la sita, huku ikilenga kuimarisha zaidi kwenye Kusoma, Kuandika na kuhesabu na stadi nyengine za maisha. Mtaala unamtaka mwanafunzi anaeanza kujiunga na shule ya msingi kuanza darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka sita (6) huku akimaliza elimu yake ya msingi yaani darasa la sita akiwa na miaka kumi na moja (11). Kwenye upande wa darasa la tatu mpaka la sita maeneo ya kujifunza na masomo yamezingatia kumjengea mwanafunzi umahili wa lugha na mawasiliano, sayansi ya jamii, sayansi na teknolojia, hisabati, sanaa na michezo. Kwa upande wa lugha wanafunzi watajifunza lugha za Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa, Kichina na Kiarabu.

RELATED ARTICLES

Most Popular