Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa taasisi zote kutumia namba moja tu ya NIDA ili kurahisia huduma na taarifa.
Amewataka Mabenki, Wizara ya Elimu, Wizara ya Afya na wizara nyengine zote zinazotoa huduma, sasa wakatumie namba moja tu Mtanzania (NIDA), Hii itasaidia taarifa za Mtanzania mwenye namba husika kupatikana kirahisi kwenye kila taasisi na kupunguza usumbufu wa kutoa taarifa tena badala yake ni kuingiza namba na kuonesha taarifa za muhusika.
Pia amesisitiza Mtazania akizaliwa tu anapopata cheti cha kuzaliwa basi na namba yake ya NIDA itoke na taarifa zake zianze kukusanywa wakati ule ule Jina lake, Jinsia, Hospitali aliyozaliwa n.k