Gazeti la MwanaHalisi pamoja na Mhariri wake Saed Kubenea wametakiwa kuomba radhi ndani ya siku 14.
Dk. Jakaya Kikwete ambae ni Rais mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wametoa siku 14 za kuomba pamoja na kufuta kashfa iliyochapishwa na Gazeti hilo ikiwatuhumu viongozi hao kufadhili wanaopinga Mkataba wa DP World na TPA.
Wakili Eric Ng’maryo amesema Gazeti hilo la MwanaHalisi lilichapisha taarifa za Uongo dhidi ya Kikwete na Kinana, na endapo uongozi wake hautaomba radhi na kuchapisha taarifa ya kufuta kashfa hizo, Viongozi hao watachukua hatua za Kisheria.