Saturday, May 18, 2024
HomeTop NewsMO Dewji atoa malalamiko viongozi Simba

MO Dewji atoa malalamiko viongozi Simba

Mohammed Dewji almaarufu MO leo 10, Agosti 2023 ametoa malalamiko yake kwa Wana Simba kuhusiana na swala la kunyimwa Tiketi ya VVIP ya mtoto wake.

Kupitia mtandao wa X (zamani Twitter) Mo Dewji amechapisha kwenye akaunti yake ujumbe huu “Wanasimba nawapenda sana, ila naomba kulalamika, nimeomba ticket ya VVIP kuajili ya mtoto wangu: kamati ya Salim Mk wa board na pamoja na Mk wa simba Mwangungu na CEO Imani wamekataa. :- Je hii ni haki? je hi ni zhulma?” mwisho wa kunukuu.

Aidha mapema kabla ya post hiyo MO alichapisha kiasi alichotoa ili kufanikisha usajili uliofanya na klabu hiyo hivi karibuni, ambapo amesema ametoa karibu shilingi za Kitanzania Bilioni tatu (3) huku akikazi kwamba asitokee mtu akasema kwamba MO hajatoa hela na kuwataka kuepukana na wapotoshaji.

RELATED ARTICLES

Most Popular