Thursday, December 7, 2023
HomeTop NewsMahakama yabariki uwekezaji Bandarini

Mahakama yabariki uwekezaji Bandarini

Mahakama Kuu kanda ya Mbeya leo imetoa hukumu ya kesi iliyofunguliwa na Wakili Boniface Mwabukusi na wenzake, kwenye kesi hiyo ambapo upande wa walalamikaji / wafungua mashtaka walipeleka ombi la kupinga mkataba wa bandari baina ya serikali ya Dubai ikiwakilishwa na kampuni ya DP World na Serikali ya Tanzania chini ya Tanzania Port Authorities (TPA).

Mahakama hiyo imetupilia mbali kesi hiyo na kusema malalamiko yaliyowasilishwa hayana mashiko.

Aidha kwa upande wa waleta maombi wamesema wanaenda kukata rufaa baada ya kukamilisha taratibu za kisheria kwa kuwa hawajaridhika na maamuzi ya Mahakama hiyo.

RELATED ARTICLES

Most Popular