Saturday, May 18, 2024
HomeTop NewsSpika Mh. Dkt Tulia awataka vijana kujitengenezea Ajira za kudumu

Spika Mh. Dkt Tulia awataka vijana kujitengenezea Ajira za kudumu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amewataka Wananchi hususani vijana kutumia fursa ya uwekezaji katika kilimo ili kujitengenezea ajira ya kudumu.

Dkt. Tulia ameyasema hayo leo tarehe 4 Agosti, 2023 wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho ya Wakulima na Wafugaji (Nane-Nane) yanayoendelea katika viwanja vya John Mwakangale Jijini Mbeya.  

Ameongeza kuwa ni wajibu wa kila Mwananchi kuungana na Serikali katika kutimiza azma ya kufanikisha mapinduzi ya kilimo nchini yanazaa matokeo chanya.  

“Serikali yetu inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejitahidi kuwekeza na kuwawezesha vijana kujikita katika kilimo ikiwemo uanzishwaji wa mradi wa mashamba makubwa ya kuwezesha vijana kulima kibiashara (BBT) hivyo basi hakuna budi kila mmoja kuona ipo tija ya kushiriki katika uwekezaji huu” Amesisitiza Dkt. Tulia

RELATED ARTICLES

Most Popular