Wednesday, July 17, 2024
HomeTop NewsHotel ya Karibu Beach Resort yateketea kwa moto

Hotel ya Karibu Beach Resort yateketea kwa moto

Hotel ya Karibu Beach Resort iliyopo Pongwe Unguja imeteketea kwa moto huku chanzo cha moto huo ni shoti ya umeme.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadid Rashid amesema limetoka Jioni ya leo tarehe 3 Agosti 2023, ambapo moto huo ulianzia kwenye vibanda vya makuti jirani na Hotel hiyo, kutokana na upepo mkali ukasababisha kusambaa kwa moto huo mpaka kwenye hoteli hiyo na kuteketeza kila kitu.

Akizungumzia madhara yaliyotokea baada ya ajali hiyo Mkuu wa mkoa amesema Wageni wote wapo salama ila mmoja amepoteza Hati yake ya kusafiria (Passport) huku watatu wakiwa wameunguliwa na vitu vyao vyote. Kwa upande wa Hotel jumla ya vyumba 15 vimeshika moto na kuathiriwa.

RELATED ARTICLES

Most Popular